Iran, IAEA kuanza mazungumzo mapya

CAIRO,MISRI : WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, anatarajiwa kukutana kesho na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, katika kikao cha kwanza tangu Tehran kusitisha ushirikiano na shirika hilo miezi miwili iliyopita.
Mazungumzo hayo, yatakayoshirikisha pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty, yanatazamiwa kujadili itifaki mpya ya ushirikiano kati ya Iran na IAEA. Hatua hiyo inafuatia lawama zilizotolewa na Iran dhidi ya IAEA kwa kushindwa kulaani mashambulizi ya Marekani na Israel yaliyolenga mitambo yake ya nyuklia mwezi Juni. SOMA: Iran kuendeleza mazungumzo IAEA
Wakati huo huo, mataifa ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani yameanzisha mchakato wa kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa, yakieleza kutoridhishwa na utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015.
I just got paid $22k working off my laptop this month!** And if you think that’s cool, my divorced friend has twin toddlers and made over $22620 her first month. details on this website**Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA……..
Here is I started_______ https://Www.CashHive1.Com