Iran, IAEA yafikia makubaliano mapya

CAIRO, MISRI : IRAN imekubaliana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kudhibiti Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (IAEA) kuhusu mfumo mpya wa ushirikiano, hatua inayochukuliwa baada ya kusimamisha ushirikiano wake kufuatia mzozo na Israel mwezi Juni.
Makubaliano hayo yaliidhinishwa mjini Cairo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, pamoja na Mkuu wa Shirika la IAEA, Rafael Grossi, ambaye alisifu hatua hiyo kama “hatua muhimu katika mwelekeo sahihi.” SOMA: Iran, IAEA kuanza mazungumzo mapya
Huu ulikuwa mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu kati ya Iran na IAEA tangu kuahirishwa kwa ushirikiano wao kufuatia vita vya siku 12 na Israel, ambapo Israel na Marekani zilisababisha mashambulizi kwenye vinu vya nyuklia vya Iran.
Wakati wa mkutano huo mjini Cairo, Waziri Araghchi na Grossi walikutana na Rais wa Misri, Abdelfattah al-Sisi, ambaye aliyepongeza makubaliano hayo kama “hatua chanya kuelekea kudhibiti silaha za nyuklia.”
Makubaliano haya yanaashiria jitihada mpya za kidiplomasia katika kudhibiti mzozo wa nyuklia Mashariki ya Kati, huku dunia ikifuatilia kwa karibu hatua za Iran na IAEA.
Google pays $300 on a regular basis. My latest salary check was $8600 for working 10 hours a week on the internet. My younger sibling has been averaging $19k for the last few months, and he constantly works approximately 24 hours. I’m not sure how simple it was once I checked it out.
This is my main concern……………………………. http://Www.Cash43.Com