Iran kuendeleza mazungumzo IAEA

TEHRAN : SERIKALI ya Iran imesema itaendelea na mazungumzo na Shirika la Kudhibiti Nyuklia la Umoja wa Mataifa (IAEA), licha ya mvutano wa kidiplomasia ulioibuka miezi ya karibuni.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, amesema awamu nyingine ya majadiliano imepangwa kufanyika hivi karibuni. Iran ilisitishe ushirikiano wake na shirika hilo baada ya kumalizika kwa vita vya siku 12 kati yake na Israel mnamo Juni, ambapo Marekani na Israel zilivishambulia vituo vya nyuklia vya Tehran.

Mnamo Juni 25, siku moja baada ya mapigano hayo kusimamishwa, wabunge wa Iran walipiga kura kwa pamoja kusitisha shughuli za IAEA nchini humo. SOMA: Iran yatoa masharti mapya ya Nyuklia

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button