Israel yaamuru wakaazi Gaza kuondoka

GAZA, PALESTINA : JESHI la Israel limewaamuru wakaazi wa jiji la Gaza kuondoka mara moja, wakati likijiandaa kuanzisha mashambulizi mapya dhidi ya ngome za kundi la Hamas. Agizo hilo limetolewa sambamba na onyo kali kwamba oparesheni hizo za kijeshi zitaendelea endapo Hamas haitawaachilia huru mateka waliobaki.

Inakadiriwa kuwa wakaazi wapatao milioni moja wameendelea kuishi kwa hofu kubwa, hasa baada ya Israel kutangaza mpango wa kuliangamiza kundi la Hamas tangu vita vilipozuka Oktoba, 2023. Hata hivyo, agizo hilo limeibua taharuki kubwa miongoni mwa wakaazi. Baadhi yao wamelazimika kuelekea maeneo ya kusini mwa Gaza, huku wengine wakisisitiza kubaki jijini humo kwa madai kwamba hakuna eneo salama la kukimbilia.

Kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu, wakazi wa Gaza tayari wamehamishwa mara kadhaa tangu kuanza kwa vita, wakihama kati ya kaskazini na kusini mwa ukanda huo. Hali hiyo imezidisha janga la kibinadamu na kusababisha baa la njaa inayohatarisha maisha ya maelfu ya Wapalestina. SOMA: Hamas yakubali kusitisha vita Gaza

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button