MAREKANI : SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeishtumu Israel kwa mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza wakati wa vita na Hamas.
Shirika hilo limesema Israel imefanya hivyo kutaka kuwaangamiza Wapalestina kwa kufanya mashambulizi , kubomoa miundombinu muhimu na kuzuia kupelekwa kwa chakula, dawa na misaada mingine katika Ukanda wa Gaza.
Ripoti hiyo imesema mauaji haya hayawezi kuhalalishwa na shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023 dhidi ya Israeli, ambalo lilichochea kuzuka kwa vita hivyo.
Mkuu wa shirika hilo Agnès Callamard amesema, ”Israel limefanya na linaendelea kufanya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 2023 siku ambayo Hamas ilifanya uhalifu wa kutisha dhidi ya raia wa Israel na watu wengine”,
Aliongezea,“Wapalestina wa Gaza wanaishi kwa hofu huku mauaji ya watu yakiendelea kutokea mbele yao na hakuna dalili ya kumalizika.”Alimalizia Agnes.
SOMA: UN yaridhia Israel kuondoka Palestina
Inadaiwa kuwa Marekani na washirika wengine wa Israel wanaweza kuhusishwa na mauaji ya halaiki na kuwataka kuacha kutoa silaha kwa Israel.