Maelfu waandamana kuunga mkono Palestina

ITALIA : MAELFU ya watu nchini Italia wamejitokeza mitaani kushinikiza mshikamano na raia wa Palestina walioko Gaza. Waandamanaji hao walikusanyika katika miji kadhaa ikiwemo Milan na Roma, ambapo baadhi yao walivamia kituo kikuu cha treni na kukabiliana na polisi.

Miongoni mwa watu walioshiriki maandamano hayo ni walimu, mafundi vyuma na wafanyakazi wa sekta nyingine, vilitangaza mgomo wa saa 24 uliosababisha usumbufu mkubwa. Shughuli za usafiri wa umma, shule na bandari zilitatizika huku treni za masafa marefu zikichelewa kwa muda mrefu.

Takriban watu 20,000 walikusanyika nje ya kituo kikuu cha Roma wakiilalamikia uvunjifu wa haki za binadamu katika ukanda wa Gaza. Waandamanaji wametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua za dharura kukomesha mapigano kati ya Israel na Palestina. SOMA: CHP yaitisha maandamano makubwa Istanbul

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button