Ivory Coast, Tanzania zapanda viwango Fifa
Mabingwa wa soka Afrika, Ivory Coast wamepanda nafasi 10 kwenye viwango vipya vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) vilivyotangazwa leo Februari 15, 2024.
Timu hiyo imepanda kutoka nafasi ya 49 hadi nafasi ya 39, ikiwa ni baada ya kushinda kombe la mataifa ya Afrika (Afcon) Februari 11, mwaka huu.
Katika viwango hivyo pia timu za ukanda wa Kaskazini mwa Afrika za Algeria, Misri na Tunisia zimeshuka. Misri wameshuka kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya 33 hadi nafasi ya 36 huku Algeria na Tunisia zikishuka kwa nafasi kumi. Tanzania imepanda kwa nafasi nafasi mbili kutoka nafasi ya 121 hadi 119.