Jamii iunge mkono mikakati kuwalinda watoto nchini

SHERIA ya Mtoto ya Mwaka 2009 na marekebisho yake pamoja na Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977 vinaeleza mtoto ni raia yeyote wa Tanzania mwenye umri chini ya miaka 18.
Sheria mama (Katiba) na nyingine zinazomuhusu mtoto, zinatoa haki kwa mtoto kupata mahitaji muhimu kutoka kwenye familia ikiwemo malazi, chakula, mavazi, matunzo, ulinzi, usalama na kusikilizwa.
Misingi ya sheria hizi ni hakikisho ya haki za watoto zinazopaswa kutekelezwa na jamii ili mtoto wa Kitanzania aweze kuishi kwa amani na kufikia ndoto zake za kuwa raia mwema wa sasa na baadaye.
Kutokana na umuhimu huo, halmashauri mbalimbali ikiwemo Jiji la Dodoma zimeandaa mpango mkakati wa kuelimisha jamii ili kuhakikisha watoto wanalindwa, wanaenda shule na kuepuka mazingira hatarishi ya ajira zisizo rasmi.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Wilaya ya Dodoma, alinukuliwa hivi karibuni akieleza kuhusu mkakati huo katika kikao cha mkakati wa kutoa elimu juu ya madhara ya ajira kwa watoto.
Tunaamini mpango mkakati huo wa kutoa elimu zaidi kwa jamii utasaidia jamii kuachana na dhana ya kuwatumikisha watoto na badala yake itawapa nafasi ya kusoma na kulinda haki zao.
Mpango mkakati huo wa kutoa elimu tunashauri ujikite katika uelewa na kinga, uweke bayana madhara na hatari ya kutowalinda watoto kiroho na kimwili ili jamii ibebe dhamana hii kwa pamoja.
Tunaikumbusha jamii kuwa ni wajibu wake kushirikiana na serikali na asasi za kiraia kuelimisha madhara ya ajira za watoto kwani ni sehemu ya ukatili unaosababisha wakose haki ya elimu na kutunzwa.
Jamii ikishiriki kwa karibu mipango hii ya kuwalinda watoto itakuwa na tija na watoto watajengewa msingi imara wa maisha yao ya baadaye na ustawi wa taifa.
Katika hili, tunashauri wazazi wawe mstari wa mbele kufuatilia kwa karibu maisha ya watoto nyumbani, mtaani, shuleni na wakiwa kwenye nyumba za ibada kuhakikisha wanakuwa salama.
Tunahimiza kila halmashauri nchini iwe na mkakati wa kulinda watoto dhidi ya athari hasi za maendeleo ya kidijiti ili kujenga taifa imara la baadaye.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com