Jamii Lindeni Watoto – Rosa Ree

DAR-ES-SALAAM: Msanii wa miondoko ya  ‘Hip Hop,   Rosary Iwole maarufu ‘Rosa Ree’ ameungana na Watanzania kusikitika na kukemea wimbi la kupotea kwa watoto hapa nchini.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Rosa Ree ambaye ni mama wa mtoto mmoja, amesema kuwa anajiuliza maswali nani atawalinda watoto.

Amesema watoto wanapokwenda shuleni wanatokea ‘maanti’ wasiojulikana wamekuwa wakijitokeza bila idhini ya  wazazi  na kuwachukua na kwenda kuwafanyia vitendo vya ukatili kwa kuwabaka, kulawiti na kuwachinja.

Advertisement

“Tuwafiche wapi watoto wetu na ndio future yetu. Lakini dunia ya sasahivi imekua na uovu usiokua na hata huruma hata kwa watoto,” alimalizia.

SOMA: Samia kugharamia tiba mtoto aliyenusurika kuchinjwa

Aliongezea “Kumbaka/kumlawiti mtoto sio hamu ni Ushetani! Kumteka mtoto kumtoa viungo na kuviuza sababu sio umaskini ni Ushetani”.alimalizia.

Pia amewaomba watanzania  kushikamana katika kuwalinda watoto  kwa kuangalia hali sawa kwa wazazi wenye vipato na wasio na vipato.

“Tuwafiche wapi watoto wetu tupaze sauti zetu mpaka sauti yetu kwa pamoja kama jamii isikike,” alimalizia.

SOMA: https://www.jamii.go.tz/