ZANZIBAR: Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi DCP ZUBERI CHEMBERA ameitaka jamii kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kupunguza uhalifu wa makosa mbalimbali yakiwemo ya Mauaji, udhalilishaji na wizi ambayo yamekuwa yakijitokeza kwenye jamii.
Akitoa tathimini ya hali ya Uhalifu kamisheni ya Polisi Zanzibar kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2024 katika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar DCP CHEMBERA amesema Jumla ya Makosa makubwa 1,652 ya Jinai yameripotiwa ikilinganishwa na makosa 1,459 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho mwaka 2023 kukiwa na ongezeko la makosa 193 sawa na asilimia 13.2.