Jela maisha kwa kumnajisi mwanafunzi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha imemfunga kifungo cha maisha Ole Sure Miliari mwenye umri wa (19) kifungo cha maisha jela mara baada kukutwa na hatia ya kumnajisi mwanafunzi wenye umri wa miaka 8 mkazi wa wilaya hiyo.

Kesi hiyo namba 16 ya mwaka huu 2023 mtuhumiwa alitenda kosa hilo katika Wilaya ya Ngorongoro  la kumlawiti mwanafunzi wa shule ambapo mara baada ya uchunguzi wa daktari aligundulika mwanafunzi huyo aliharibika vibaya katika maumbile yake nakupelekea kufungwa nepi kutokana na kitendo hicho.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya Ngorongoro, Kohawa Mboya alisema kuwa Olesule amekutwa na hatia baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa Jamhuri na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo na mtumiwa kukutwa na hatia hivyo kupelekea kupata adhabu kali ya kifungo cha maisha.

Advertisement

Hakimu Mboya alisema kuwa adhabu hiyo iwe fundisho kwa wale wote wenye vitendo vibaya ambavyo avikubaliki katika  jamii na vinaendana  kinyume na maadili ya Mtanzania .

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Mimutie Women Organization,Rose Njilo amesema kuwa wao kama taasisi ya kutetea haki za wanawake na watoto wameishukuru mahakama hiyo kwa kutenda haki kwani adhabu hiyo itarudisha maadili kwa jamii na kuwa fundisho kwa wengine wenye tabi la za namna hiyo .

Aidha Rose Njilo ameishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wao ambao wamefanya mpaka kupelekea mtuhumiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani na kukiri makosa kwamba ni kweli alifanya kitendo cha ulawiti kwa mwanafuzni  huyo .

Rose ametoa wito kwa jamii kuachana na tabia mbaya ya vitendo vya ulawiti hasa katika jamii ya kifugaji ambayo inaonekana kudumisha maadili ya kitanzania ikilinganishwa na baadhi yao kuingia katika vitendo  hivyo kinyume na maadili

Pia ametoa shukrani zake kwa taaasisi ya Women Fund Tanzania kwa kuendelea kuwa wawezeshaji wa Shirika la Mimutie katika kuibua changamoto za ukatili wa kijinsia ndani ya jamii ya Tanzania .

Wadau mbalimbali na wanaharakati walifika katika mahakama hiyo kusikiliza hukumu hiyo na kusema kuwa mahakama imetenda haki kwa mshtakiwa na mshitakiwa hakuisumbua mahakama kwamba akufanya tendo hilo la ulawiti kwa mwanafuzi wa miaka 8 bali alikiri kosa ambalo baadae alikuja kulijutia.

1 comments

Comments are closed.