Jela miaka 30 kwa kumbaka ajuza

WANGING’OMBE, Njombe: MAHAKAMA ya Wilaya ya Wanging’ombe Mkoa wa Njombe imemhukumu Elias Thomas Mwanzalila (miaka 30) mkazi wa Mtaa wa Igima kwenda jela miaka 30 kwa kosa la ubakaji wa bibi kizee mwenye umri wa miaka 81.

Mtuhumiwa ametenda kosa hilo Februari 19,2024 huko Wanging’ombe Mkoa wa Njombe.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu, Jaji Jamsi Emmanuel Mhone amesema Mahakama imejiridhisha kwa ushahidi uliotolewa na kumkuta mtuhumiwa na hatia hiyo ya ubakaji.

Soma pia: https://habarileo.co.tz/aliyehukumiwa-miaka-30-jela-kwa-ubakaji-aachiwa/

Hivyo, Mahakama imemhukumu miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo vya ukatili.

Soma pia: https://www.instagram.com/p/C7TZqVYsKUi/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

Habari Zifananazo

Back to top button