Jela mwaka mmoja kwa wizi wa pikipiki

MBEYA: MAHAKAMA ya Mwanzo Ndobo, wilayani Kyela mkoani Mbeya, imemhukumu Jey Mwamakula (26), mkazi wa Ipinda, kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa pikipiki yenye thamani ya Sh milioni 3.4.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa mahakama hiyo, Kogile Chamani, baada ya mahakama kujiridhisha na ushahidi uliowasilishwa kuhusu tukio hilo.

Awali, mahakama ilielezwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Novemba 8, 2026, majira ya saa 2 usiku, kwa kuiba pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usajili MC 269 FNH.

Ilidaiwa kuwa usiku huo mshtakiwa aliingia ndani ya nyumba ya mlalamikaji na kuchukua pikipiki hiyo, kisha kuipeleka kwa fundi kwa lengo la kubadilisha muonekano wake ili iwe vigumu kutambulika kabla ya kuiuza.

Hata hivyo, akiwa kwa fundi huyo, alitiliwa shaka na hatimaye kukamatwa na kufikishwa kituo cha polisi kwa hatua za kisheria.

Msimamizi wa Mahakama, Sajenti wa Polisi Emmanuel Chakalike, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa, akieleza kuwa ni mkosaji wa kujirudia katika makosa ya wizi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button