Jengo la serikali lashambuliwa Kyiv

KYIV, UKRAINE: JENGO kuu la serikali ya Ukraine huko Kyiv limepigwa kwa mara ya kwanza katika vita dhidi ya Urusi, amesema Waziri Mkuu Yulia Svyrydenko. Amesema paa na gorofa la juu vimeharibiwa, huku takriban watu wanne wakiuawa, akiwemo mtoto mchanga na mwanamke baada ya jengo la ghorofa tisa kugongwa katika wilaya ya Svyatoshynsky.

Jeshi la anga la Ukraine limesema zaidi ya ndege zisizo na rubani na makombora 800 yamezinduliwa na Urusi. Kati ya vifaa hivyo, makombora tisa na ndege zisizo na rubani 56 viliwashambulia maeneo 37, huku vifusi vingi vikidondoka katika maeneo manane, ikisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu.

Rais Volodymyr Zelensky alisema mashambulio yamesababisha uharibifu katika miji ya Zaporizhzhia, Kryvyi Rih na Odesa, pamoja na mikoa ya Sumy na Chernihiv. “Mauaji kama haya ni uhalifu wa makusudi na jaribio la kurefusha vita,” alisema.

Hatahivyo Wizara ya Ulinzi ya Urusi imethibitisha kufanya shambulio hilo na kudai kuwa shambulio hilo limefanywa kwenye jengo la kijeshi, viwanda na miundombinu ya usafirishaji, na kusababisha uharibifu wa silaha na vifaa vya kijeshi. SOMA: Marekani yaitaka Urusi kusitisha mapigano

Habari Zifananazo

8 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button