Jeshi latangaza nafasi za ajira

DODOMA: Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya sekondari hadi elimu ya juu.

Aidha, uandikishaji utahusisha vijana wenye taaluma adimu huku waombaji wakitakiwa kuhakikisha maombi Yao yanaandikwa kwa mkono.

Akizungumza na waandishi wa habari jana makao makuu ya Jeshi jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania, Kanali Gaudentius Ilonda alisema maombi yanapaswa kuwasilishwa makao makuu ya Jeshi kwa njia ya mkono au kwa sanduku la posta kuanzia leo Mei Mosi hadi Mei 14 mwaka huu.

“Wataalam watakoandikishwa Jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali muhimu ya kijeshi na mafunzo ya kuwaendeleza katika taaluma zao.”

Aidha, Kanali Ilonda alitaja sifa za vijana waombaji wa nafasi hizo kuwa ni lazima awe raia wa Tanzania mwenye kitambulisho cha Taifa, mwenye afya nzuri na akili timamu na mwenye tabia na nidhamu nzuri, ambaye hajapatikana na tabia ya makosa ya jinai.

Alisema pia awe na cheti halisi cha kuzaliwa, vyeti vya shule na vyeti vya taaluma na awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Cha Kuzuia Magendo na awe amehitimu mafunzo ya Jeshi la Kujega Taifa kwa mkataba wa kujitolea au Mujibu wa Sheria na kutunukiwa cheti.

“Kwa vijana wenye elimu ya Kidato Cha Nne na Kidato Cha Sita awe na umri usiozidi miaka 24, kwa vijana wenye elimu ya stashahada awe na umri usiozidi miaka 26, kwa wenye elimu ya juu uliwao usizidi miaka 27 na madakitari bingwa wa binadamu umri wao usizidi miaka 35.”

Aidha, Kanali Ilonda alisema vijana wanaohitajika kuandikishwa Jeshini ni wataalamu wa tiba ambao ni wabobezi, general surgeon, orthopaedic Surgeon, Urologist Radiologist, ENT Specialist, Anaesthesiologist, physician, Ophthalmologist, paediatrician, obstetrician & Gynaecologist, oncologist, pathologist, psychiatrist, emergency medical specialist na haematologist.

Alisema kundi la pi la wataalamu wa tiba ni medical doctor, dental doctor, veterinary medicine, bio medical engineer, dental laboratory technician, Anaesthetic, Radiographer, optometry, physiotherapy na aviation doctor.

Kwa upande wa taaluma za uhandisi. Kanali Ilonda alisema ni wenye shahada ya electronic engineering, mechanical engineering, marine engineering, marine transportation & nautical science, mechanical in marine diesel engine, aviation management.

Pia wenye shahada ya aircraft accident & incident investigation, meteorogy, Air Traffic Management & aeronautic engineering.

Kanali Ilonda alisema pia wanaohitajika ni mafundi mchundo wa aluminium welding na welding and metal fabrication.

“Maombi yate yaandikwe kwa mkono na yawasilishwe kwa mkono au kwa njia ya posta makao makuu ya Jeshi Dodoma kuanzia Mei 1(Leo) hadi Mei 14 mwaka huu yakiwa na viambatisho ambayo ni nakala ya kitambulisho cha Taifa au namna ya NIDA, nakala ya cheti cha kuzaliwa, vyeti vya shule na Chuo na nakala ya cheti cha JKT kwa waombaji waliomaliza mkataba wa kujitolea na kuweka namba ya simu ya mkononi ya mwombaji.”

“Maombi yatumwe kwa Mkuu wa Utumishi Jeshini, Makao Makuu ya Jeshi, sanduku la posta 194, Dodoma, Tanzania.”

Kanali Ilonda alisisitiza kuwa: ”idadi ya vijana watakaoandikishwa Jeshini itategemea waliokidhi vigezo na masharti yaliyowekwa, tuwatangazie wananchi watume maombi kwa kuwango cha elimu alichonacho kwani elimu zote zinatakiwa ili mradi akidhi vigezo na nisisitize kupitia JKT sio guarantee ya kuandikishwa jeshini.”

Akijibu swali ni kwa nini wametoa fursa mkubwa kwa wataalamu wa tiba, alisema hatua imelenga kupanua wigo na kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika hospitali za Jeshi kwa kuwahudumia wanajeshi, familia za askari na wananchi wanaozunguka huduma hizo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button