Jimmy Carter kuzikwa 9 Januari 2025

MAREKANI : MAZISHI ya kitaifa ya Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter yatafanyika katika Kanisa Kuu la katoliki mjini Washington Januari 9 .
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Ikulu ya White house imesema kuwa Januari 9 itakuwa siku maalum ya maombolezo ya kitaifa ya Jimmy Carter.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa siku sita za mazishi ya kitaifa zitaanza jumamosi wiki hii hadi tarehe 9 Januari ambapo atazikwa.
Jeshi nchini Marekani limesema mwili wake utasafirishwa kwa msafara wa magari kupitia mji aliozaliwa wa Plains katika jimbo la Georgia. SOMA : Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter amefariki dunia
Msafara huo pia utasimama shambani alikokulia, kisha mwili wa Carter utasafirishwa hadi Atlanta, ambako utalala katika Kituo cha Carter hadi asubuhi ya Januari 7.
Kisha baadae mwili utasafirishwa hadi Washington, DC ambako utalazwa katika majengo ya Bunge la Marekani – Capitol Hill hadi pale itakapofanyika ibada ya kitaifa ya kuuaga.
Jimmy Carter amepangwa kuzikwa Georgia Januari 9 pembezoni mwa kaburi la mke wake, Rosalynn Carter ambaye amezikwa nyumbani kwao mjini Plains.
Carter alifariki dunia mwishoni mwa wiki hii baada ya kusumbuliwa na maradhi ya muda mrefu na amefariki akiwa na umri wa miaka 100.



