JK kushiriki uzinduzi jengo la Uhamiaji Pemba

PEMBA; Rais mstaafu Awamu ya Nne wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete, akiwasili Kisiwani Pemba kwa ajili ya sherehe ya uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Uhamiaji na Makaazi ya Askari,Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Dk Kikwete amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Hassan Yahaya.
Uzinduzi huo ni sehemu ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Uzinduzi huo unafanyika leo Januari 4,2026.



