JKCI kuanza upandikizaji wa moyo rasmi

DAR ES SALAAM: TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeanza rasmi mkakati maalum wa kufanikisha huduma za upandikizaji wa moyo hapa nchini kwa kuunda kamati maalum itakayofanya kazi hiyo kwa miaka mitano.
Akizungumza leo wakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya taasisi hiyo Mkurugenzi wa JKCI, Dk Peter Kisenge Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kwa Afrika Mashariki kutoa huduma hiyo ya upandikizaji moyo.
“”Leo tunapoenda kuadhimisha miaka 10 tunaenda kufungua kamati maalum itakayokuja kufanya kazi kwa miaka mitano kufanya kazi ya upandikizaji moyo,haya ni mafanikio makubwa sana kama taasisi kupandikiza moyo.
Amesema nchi zinazofanya upandikizaji wa moyo Afrika ni pamoja na Afrika kusini,Misri na Afrika kaskazini.
“Uhitaji ni mkubwa magonjwa ya moyo yanaongezeka kwa kasi na vijana wanapata hasa magonjwa ya misuli ya moyo ambapo moyo unakuwa umechoka na ukiwa uko chini ya miaka 50 kwanini upoteze maisha mapema ndio maana sisi kama taasisi tunataka kulinda afya ya wananchi waweze kutibiwa,”amesisitiza Dk Kisenge.
Amebainisha kuwa kwa sasa wagonjwa walioko katika nchi za Afrika wakipata matatizo ya moyo kimbilio lao ni JKCI huku akitaja mafanikio hayo makubwa yametokana na ubunifu.
“Tunavyo vifaa vilivyowekwa hapa ni vikubwa ambavyo serikali imewekeza kwenye vifaa vikubwa vinavyoendana na nchi zilizoendelea kama Marekani,Uingereza na zingine na hospitali kubwa 20 duniani zinakuja kufanya huduma hapa wanakuja kwasababu ya maendeleo ya rasilimali watu na vifaa vilivyowekezwa na serikali,”amefafanua.
Dk Kisenge amesema sasa taasisi hiyo imeweza kufanya upasuaji wa kubadilisha valvu bila kupasua kifua ambapo huduma hizo zinatolewa na hospitali kubwa pekee.
“Matibabu ya moyo Duniani kote ni gharama valuvu kuwekewa ni milioni 10 na kuzibua mishipa ni milioni sita kwahiyo ni hela nyingi na serikal imefanya kazi kubwa asilimia 75 wanabima ya afya na sasa serikali imepitisha bima ya afya kwa wote sasa watu wote watapata huduma,”amesema.
Ameeleza kuwa serikali pia inautaratibu wa kutoa msamaha wa matibabu ambapo JKCI kila mwezi inatoa msamaha ya zaidi ya Sh milioni 200.
Aidha amewashukuru wadau mbalimbali wa mabenki na mashirika ya umma kwani kwa kipindi cha mwaka jana walitoa kiasi cha Sh bilioni 2.7 ambayo imeenda kuwasaidia wasio na uwezo.
“Niwaomba wanapokuwa na huo uwezo walete fedha,”amesisitiza.
Dk Kisenge amesema magonjwa ya moyo yanasababishwa na mtinfo wa maisha usiofaa kama unywaji wa pombe uliokithiri ,kutofanya mazoezi, kutokula kula vizuri,uvutaji wa sigara uliokithiri na kuwataka watanzania kufanya mazoezi.



