JKCI yazindua mifumo ya kisasa ya miadi

DAR-ES-SALAAM : TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeanzisha mifumo miwili ya kisasa ya kuweka miadi kwa ajili ya kumuona daktari na mfumo wa namna ndugu wa mgonjwa anavyoweza kumtembelea mgonjwa aliyelazwa hospitalini.
Mifumo hiyo inapatikana kupitia tovuti rasmi ya taasisi hiyo (www.jkci.or.tz) ambapo wagonjwa sasa wanaweza kuweka miadi ya kumuona daktari kwa urahisi kwa kubofya sehemu ya Appointments na kuchagua tarehe, muda pamoja na aina ya huduma wanayohitaji.
Akizungumzia mfumo huo Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tehama wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Fiona Kavishe amesema uanzishwaji wa mfumo huo umelenga kupunguza msongamano wa wagonjwa na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo. “Faida ya mfumo wa miadi ya kumuona daktari utamsaidia mwananchi kumuona daktari yoyote anayemtaka tofauti na awali ilikuwa wagonjwa baadhi wanamuona daktari huyo huyo”, amesema Fiona
Fiona amesema kupitia mfumo wa kutembelea wagonjwa waliolazwa wodini, ndugu wa wagonjwa wanaotaka kuwatembelea wagonjwa waliolazwa hospitalini wanaweza kutumia mfumo huo kwa kubofya sehemu ya Visitor kuchagua tarehe ya kuwatembelea wagonjwa na kufuata taratibu zilizowekwa.
Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Salehe Mwinchete amesema mfumo huo utawarahisishia madaktari kupanga ratiba zao vizuri na kuweza kufahamu kwa siku wana idadi ya wagonjwa wangapi tofauti na awali ilikuwa ngumu kwao kuweka ratiba zao vizuri. SOMA: JKCI yafanya kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto
Dk. Salehe amesema wagonjwa wakitumia mfumo wa miadi ya kumuona daktari kutasaidia kupunguza malalamiko ya wao kukaa muda mrefu hospitali kusubiri huduma lakini pia kutawapa muda wa kupumzika na kuacha tabia ya kuamka mapema kuwahi foleni ya kumuona daktari.
Naye mgonjwa aliyefanikiwa kufanya miadi kupitia tovuti hiyo Wenceslous Shoo alisema mfumo huo ni mzuri na una faida nyingi kwa wagonjwa kwani watakuwa na muda mchache wa kukaa hospitali. “Huduma hii ya kuweka miadi mtandaoni ni mzuri kwasababu inapunguza usumbufu wa kupanga foleni na kuamka alfajiri sana, ningeomba elimu itolewe na kuwafikia watu wengi zaidi ili waweze kuutumia mfumo huu” amesema Shoo.
Mfumo wa kidigitali wa kuweka miadi ya kumuona daktari na kutembelea wagonjwa waliolazwa JKCI umeanzishwa ili kuimarisha huduma kwa wananchi, kuongeza uwazi na kuhakikisha usalama wa wagonjwa walipoko wodini kwa kudhibiti idadi ya wageni.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com