Joyce Shebe achomoza tena TAMWA

Joyce Shebe

CHAMA  cha Waandishi Wahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) leo Agosti 27, 2022 kimefanya uchaguzi na kumchagua Joyce Shebe kuwa Mwenyekiti wa chama hicho.

Shebe ambaye ni Mhariri Mkuu wa Clouds Media Group, ataongoza kwa miaka mitatu. Huu ni muhula wa pili kwa Shebe baada ya kuongoza miaka mitatu ya mwanzo kuanzia 2019.

Katika uchaguzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Shebe alikuwa akichuana na muasisi wa TAMWA, Lyela Sheikh na kuibuka mshindi kwa kupata asilimia 57 ya kura zilizopigwa, huku mpinzani wake akipata asilimia 43.

Advertisement

Nafasi nyingine katika uchaguzi huo ni wajumbe wa bodi, ambapo Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Tumaini, Mary Kafyome, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha St.

Augustine, Dk Kaanaeli Kaale, Asha Abdi Makame na Caroline Mdundo  nao walichaguliwa kuwa wajumbe wa bodi ya TAMWA.