Jumuiya huduma za maji zaleta mapinduzi wilaya ya Geita
WAKALA wa MajiSafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Geita imeeleza kuwa Jumuiya za Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO) zimeleta mageuzi ya utoaji wa huduma hiyo.
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Geita, Mhandisi Sande Batakanwa ametoa kauli hiyo katika kikao cha nusu mwaka cha viongozi wa CBWSO kilichofanyika mjini Geita.
Amesema RUWASA wilaya ya Geita inatoa huduma katika kata 30 kati ya 37 na tayari 22 zimeshafikiwa na huduma ya maji ambapo zipo chini ya usimamizi wa CBWSO nne.
Mhandisi Sande ametaja miongoni mwa mageuzi makubwa ya CBWSO ni ukusanyaji wa mapato ya huduma ya maji ambapo jumuiya hizo zinakusanya wastani wa sh milioni 40 kwa kila mwezi.
Amesema makusanyo ya CBWSO yanasaidia siyo tu kuchangia mapato ya serikali lakini pia kuongeza upatikanaji wa fedha za dharura, matengenezo na malipo ya wasimamizi wa miradi.
Amesema CBWSO pia zimesaidia kuimarisha ulinzi wa vyanzo vya maji pamoja miradi ya maji inayojengwa na iliyokamilika na kuepusha uharibifu unaoweza kuathiri upatikanaji wa maji.
“Kwa wilaya ya Geita Ruwasa tumefikia asilimia 60 ya utoaji wa huduma ya maji, na kuanzishwa kwa Ruwasa pamoja na CBWSO kumekuwa na mapinduzi makubwa sana ya huduma ya maji”, amesema Mhandisi Sande.
Mhandisi Sande amekiri kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni uharibifu wa vyanzo vya maji unaotokana na ukataji wa miti pamoja na shughuli za binadamu hususan uchimbaji wa madini.

Ofisa Tawala wa wilaya ya Geita, Janeth Mobe amewataka viongozi wa CBWSO kushirikiana kikamirifu na viongozi wa serikali za mitaa kudhibiti uvamizi na uharibifu wa vyanzo vya maji.
Amesema CBWSO zina jukumu kubwa la kusimamia ubora wa huduma ya maji vijijini kwa kulinda miradi na kuepuka ufujaji wa mapato ya maji ili kuifanya huduma ya maji kuwa endelevu.

Meneja wa RUWASA mkoa wa Geita, Mhandisi Jabir Kayilla amesema hawapo tayari kumvumilia kiongozi wa CBWSO anayehujumu miradi na hivo kila mmoja azingatie weledi wa kazi yake.
Katibu wa CBWSO wilaya ya Geita, Lushika Robert amekiri uwepo wa changamoto kubwa ya uvamizi wa vyanzo vya maji hali inayoashiria uhitaji wa hatua stahiki ili kulinda vyanzo hivo.




I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com