JustMarkets yazindua shindano la Golden Challenge

 

KAMPUNI ya JustMarkets imezindua shindano la biashara ya masoko ya fedha lijulikanalo kama Golden Challenge, lililoanza Novemba 2, 2026 na kuisha Januari 31, 2027, likiwa na zawadi mbalimbali za dhahabu na fedha taslimu.

Shindano hilo limeandaliwa kwa ajili ya wafanyabiashara wa masoko ya fedha wenye viwango tofauti vya uzoefu, likitoa fursa za kujishindia zawadi kupitia droo za kila wiki na zawadi kubwa zitakazotolewa mwishoni mwa mashindano.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, wateja wanaostahili kushiriki ni wale wenye akaunti halisi za biashara za MT4 au MT5 na ambao watakuwa wamejiandikisha kupitia akaunti zao binafsi katika mfumo wa JustMarkets.

Ili kushiriki, mteja anatakiwa kuwa na salio la angalau dola za Marekani 100 katika akaunti yake wakati wa kujiunga na shindano, pamoja na kufanya biashara zenye jumla ya kiwango cha chini cha lots tatu katika kipindi cha mashindano.

Katika droo za kila wiki, washiriki watakaofanya angalau miamala mitatu ndani ya wiki husika watapata nafasi ya kushiriki kuwania zawadi.

Kila wiki, washindi watano watajishindia dola 200 kila mmoja. Kampuni imesema kiwango cha lots alizofanya mshiriki hakitaathiri nafasi yake ya kushinda katika droo hizo.

Aidha, washiriki 15 watakaofanya biashara kwa kiwango kikubwa zaidi watapata zawadi za dhahabu kulingana na nafasi zao kwenye orodha ya washindi.

Washiriki watakaoshika nafasi ya kwanza hadi ya tatu watapata gramu 20 za dhahabu kila mmoja, nafasi ya nne hadi ya nane watapata gramu 10, huku watakaoshika nafasi ya tisa hadi ya 15 wakipata gramu tano kila mmoja.

Pia kutakuwa na droo ya mwisho kwa washiriki watakaofanya biashara zenye jumla ya lots 10 au zaidi katika kipindi chote cha mashindano. Zawadi zitakuwa dola 1,000 kwa waliofanya lots 100 au zaidi, dola 500 kwa lots 50 hadi 99 na dola 300 kwa lots 10 hadi 49.

JustMarkets ni kampuni ya kimataifa inayotoa huduma za biashara ya mikataba ya tofauti za bei (CFDs) katika masoko mbalimbali ya fedha.

Hata hivyo, biashara ya Forex na CFDs ina hatari kubwa ya kifedha na inaweza kusababisha hasara ya mtaji uliowekezwa. Masharti na vigezo vya shindano vinatumika.

Washiriki wanashauriwa kusoma masharti kamili kupitia tovuti ya kampuni: https://justmarkets.com/trading/promotions/golden-challenge-2026/.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button