Kabudi: Tuithibitishie dunia utulivu Tanzania

SERIKALI imesema waandishi wa habari wana jukumu la kuithibitishia dunia kwamba Tanzania ni taifa lenye umoja, amani na utulivu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amesema hayo Mbeya wakati akizungumza na waandishi wa habari, vyombo vya ulinzi na usalama kwenye mkutano wa wadau wa habari na utangazaji kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Profesa Kabudi alisema wakati huu wa uchaguzi waandishi wa habari waijulishe dunia Tanzania ni taifa linalojali maendeleo ya watu wote bila kujali dini, kabila wala kipato cha mtu.

Alisema ni wakati wa kuieleza dunia kwamba Tanzania ni taifa lenye watu waliokomaa kisiasa wanaoweza kuvumiliana.

“Ninyi mmekuwa ni kiungo cha mshikamo wa taifa tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere hadi sasa kwa kuwafanya Watanzania mshikamane hata wakati wa majanga mbalimbali yanayoikabili nchi,’’ alisema Profesa Kabudi.

Aliongeza: “Ninyi mna jukumu kubwa kwanza la kuwaelimisha wananchi kuhusu haki ya kujitawala na umuhimu wa taifa letu kujitawala na taifa letu ni taifa huru lenye haiba na hulka yake, tabia, utamaduni, mila, desturi, mwelekeo alama ambao kwa wengine inaweza ikaonekana si muhimu lakini kwetu likawa jambo lenye umuhimu mkubwa”.

Profesa Kabudi alisema amani ya nchi ni msingi wa mambo yote na inazaliwa na ustahimilivu. Alisema mtu akiwa mstahimilivu haimaanishi ni mnyonge au dhaifu.

Alisema yeyote anayetoa kauli mbaya inayoweza kuvunja amani si mzalendo na hajui umuhimu wa amani.

Profesa Kabudi alisema msingi wa amani ni maelewano, ndiyo maana taifa limekuwa miongoni mwa mataifa yanayosisitiza maelewano na majadiliano.

Alisema ushirikiano wa Jeshi la Polisi na waandishi wa habari katika maandalizi ya uchaguzi mkuu yanaakisi dhamira ya serikali ya kukuza demokrasia, kudumisha haki, kuendeleza amani na kuimarisha uwajibikaji.

Profesa Kabudi alisema moja ya kazi za vyombo vya habari ni kusimamia na kulinda fahari ya maendeleo ya nchi kwa sababu kwa sasa nchi imepiga hatua kubwa ya maendeleo.

“Moja ya kazi yenu hasa katika kipindi hiki ni kueleza mafanikio makubwa na maendeleo ya nchi kwa sababu hiyo ni fahari ya nchi na Tanzania ndiyo taifa la kwanza kutambua kuwa huwezi kuwa na maendeleo bila kushirikisha wananchi,’’ alisema.

“Uchaguzi wetu ni jambo la muhimu katika kutekeleza na kudumisha demokrasia yetu,” alisema.

Aliongeza, “hata miaka ambapo kulikuwa na wasiwasi kwamba uchaguzi usingefanyika mfano Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1980 shinikizo lilikuwa kubwa kwa uchaguzi usifanyike kwa sababu nchi ilikuwa imetoka katika vita ya kupambana na Idd Amini lakini bado uchaguzi ulifanyika.”

Profesa Kabudi alisema tangu ulipoanza uchaguzi wa vyama vingi kuanzia 1958 hadi 1962 na uchaguzi wa chama kimoja 1965 mpaka 1985, bado Watanzania waliendelea kusema ni wamoja kwa sababu wanaamini kwenye demokrasia.

Alisema moja ya vielelezo vya demokrasia katika nchi yoyote ni wananchi kuwa na uwezo, haki na wajibu wa
kuchagua viongozi wao kila baada ya kipindi fulani.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I make over thirty k a month working part-time. I kept hearing from other people telling me how much money they could make online, so I decided to find out. Well, it was all true and it completely changed my life.

    This Is Where I Started……….www.get.money63.com

    1. I make over thirty k a month working part-time. I kept hearing from other people telling me how much money they could make online, so I decided to find out. Well, it was all true and it completely changed my life.

      This Is Where I Started………. W­­w­­w­­.­­C­­a­­r­­t­­B­­l­­i­­n­­k­­s­.C­­o­­m

  2. I make over thirty k a month working part-time. I kept hearing from other people telling me how much money they could make online, so I decided to find out. Well, it was all true and it completely changed my life.

    This Is Where I Started……….www.get.money63.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button