Kadogosa achukua fomu ubunge Bariadi vijijini

SIMIYU: Mgombea ubunge Jimbo la Bariadi Vijijini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Masanja Kadogosa leo Agosti 26, 2025 amechukua fomu ya kuteuliwa kugombea nafasi hiyo na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Kadogosa akiwa ameambatana na wasaidizi wake na baadhi ya wanachama wa chama hicho, amefika katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na kukabidhiwa fomu na msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Bariadi Vijijini Beatrice Gwamagombe.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Kadogosa aliongea na wananchi katika Mji wa Dutwa na kuwashukuru kwa kuendelea kumuunga mkono katika kuhakikisha anakwenda kuwatumikia kupitia nafasi hiyo.

“ Leo imekuwa siku ya kuchukua tu fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa, kazi ambayo tayari nimeifanya na tunakwenda kujaza hii fumo kisha kurudisha, kwa sasa haturuhusiwi kuongea jambo lolote,”amesema Kadogosa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button