Kadogosa amvaa mkandarasi ujenzi barabara Kahama

SHINYANGA: Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, amemtaka mkandarasi anayejenga barabara ya Kahama–Bulyanhulu JCT–Kakola yenye urefu wa kilomita 73, kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ifikapo Desemba 2026, kama ilivyoainishwa katika mkataba wa mradi huo.
Kadogosa ametoa agizo hilo akiwa Msalala, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, wakati akikagua maendeleo ya mradi huo ambao umefikia asilimia 90.17 ya utekelezaji, lakini ukiwa nyuma ya ratiba iliyopangwa.
Amesema Serikali haitatoa muda wa nyongeza kwa mkandarasi huyo na kwamba kushindwa kukamilisha mradi kwa wakati kutasababisha hatua za kimkataba kuchukuliwa dhidi yake, ikiwemo uwezekano wa kutoshiriki katika zabuni za miradi mingine nchini kwa mujibu wa taratibu.

“Sitaki kuona uzembe katika barabara hii. Nataka mnihakikishie kuwa mkataba huu utakamilika kwa muda uliopangwa. Sitaongeza muda, na mkishindwa kumaliza kwa wakati, hamtapata zabuni za miradi mingine nchini,” amesema Kadogosa.
Aidha, Waziri Kadogosa amemtaka mkandarasi huyo kuongeza mitambo, vifaa na muda wa kazi ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa shughuli zilizobaki na kuhakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati kwa manufaa ya wananchi na watumiaji wengine wa barabara hiyo.
Sambamba na hilo, Kadogosa amempa mkandarasi huyo siku 30 kurejesha mitambo yote iliyopelekwa jijini Arusha kutoka katika mradi anaoutekeleza mkoani Njombe.

Amesema atafanya ukaguzi wa vifaa hivyo ili kujiridhisha kuwa vimerejeshwa na vinatumika ipasavyo katika utekelezaji wa mradi.
Katika hatua nyingine, Waziri Kadogosa amewataka wananchi wa Msalala waliojenga ndani ya hifadhi ya barabara kuondoa majengo yao kwa hiari, akisisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watakaokiuka taratibu za hifadhi za barabara.
Kwa upande wao, Mbunge wa Msalala, Mabula Magangila, na Mbunge wa Kahama Mjini, Benjamin Ngayiwa, wamesema wananchi wanatarajia kuona barabara hiyo inakamilika kwa wakati kutokana na umuhimu wake katika kurahisisha usafiri na usafirishaji, kukuza shughuli za kiuchumi na kuchochea maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga.

Naye, Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Ntuli Mwaikokesya, amesema mradi huo unatekelezwa na kampuni ya M/s China Civil Engineering Construction Corporation (CECC) na umefikia asilimia 90.17 ya utekelezaji.
Ameeleza kuwa mradi huo uko nyuma kwa asilimia 6.85 ikilinganishwa na asilimia 97.02 iliyokuwa imepangwa kufikiwa hadi wakati wa ukaguzi, hali inayosisitiza umuhimu wa mkandarasi kuongeza kasi ya kazi ili kukamilisha mradi ndani ya muda wa mkataba.




There are certainly loads of details like that to take into consideration. That could be a nice point to carry up. I supply the thoughts above as general inspiration but clearly there are questions like the one you deliver up where the most important thing can be working in honest good faith. I don?t know if finest practices have emerged round things like that, but I am sure that your job is clearly recognized as a fair game. Each girls and boys feel the impact of just a second’s pleasure, for the rest of their lives.
❤️ Wasichana warembo na wenye hamu ya kimapenzi kutoka kote duniani wanakungoja; jiunge hapa …………………………………………………………………> https://da.gd/girls66
Really enjoying the vibe here. Everything is easy to navigate and the customer support is actually helpful. Highly recommend 56wgame for anyone starting out.