Kairuki ampongeza Uwoya kampeni ya kilimo

MSHAURI wa Rais, Ofisi ya Rais masuala ya wanawake, Angellah Angela Kairuki amempongeza mwigizaji Irene Uwoya kwa kuanzisha kampeni ya kusapoti kilimo.
Akizungumza Dar es Salaam leo kwenye utambulisho wa mradi huo Kairuki amesema Rais Samia amefanya makubwa katika sekta ya kilimo ikiwemo kuweka mazingira wezeshi wa upatikanaji wa mikopo, zana na masoko.
“Nimpongeze sana Irene Uwoya na wenzake kwa kuja na kampeni hii kwa wakati muafaka kuhakikisha kwamba wanasapoti sekta ya kilimo, niliposikia kampeni hii nilifarijika sana, nikitambua mchango wa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliofanya katika sekta ya kilimo ni mkubwa,”amesema.
Amesema Rais Samia ameweka sera bora za kuhakikisha mwanamke anashiriki katika kilimo, kuongeza uzalishaji, kuhakikisha kunakuwa na usalama wa chakula na kuhakikisha anajiwezesha kiuchumi.
Katika fedha na mikopo, amesema Rais Samia ameweka sera zilizobora kuhakikisha sekta ya kilimo inapata mikopo. Huko nyuma ilikuwa ni shida wengi walikuwa wanaitambua kilimo ni risk unaweza kuvuna au kupata hasara.
Amesema imepata bima ya kilimo kuweka mazingira wezeshi ya ulinzi, kwamba kilimo kinaendeendelea kuwa na manufaa lakini wale ambao wanafanya shughuli hizo wakiwemo wanawake kuweza kupata fedha za kufanya shughuli zao.



