KAMATI ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imeridhishwa na ujenzi wa kituo cha zimamoto kilichopo Mtumba jijini Dodoma chenye thamani ya Sh bilioni 1.9.
Akizungumza leo Novemba 18, mara baada ya kukagua mradi huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Vita Kawawa amepongeza ujenzi huo kwa kuzingatia mahitaji ya Jeshi la Zimamoto.
Awali akitoa tarifa ya ujenzi wa jengo hilo linalogharamiwa na serikali, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga, amesema ujenzi huo ulianza Aprili 2024 ambao kwa sasa umefikia asilimia 50.53, ukitumia asilimia 34.24 ya fedha zilizotolewa.
Kwa mujibu wa kamishna huyo, ujenzi wa kituo hicho utawezesha ufanisi wa jeshi hilo.
SOMA: Kwa haya, hongera Kamati ya Kudumu ya Bunge
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na mambo mengine limekuwa likikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo suala la miundombinu na vitendea kazi.