Kambi za Mbowe, Lissu zakamiana

DAR ES SALAAM; VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADE MA) Jimbo la Kibamba wamewataka wajumbe wanaoingia kwenye vikao vya Halmashauri Kuu vya chama hicho kupitia jimbo hilo, kuhakikisha wanamchagua, Tundu Lissu kuwa Mwenyekiti na John Heche  kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa katika uchaguzi utakaofanyika Januari 21, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema Kibamba, Uhuru Kitima alisema jana kuwa wanachama wa Kibamba wanamuunga mkono, Lissu na Heche kwa sababu wanaamini wataleta mabadiliko ndani ya chama.

“Kama ambavyo mnafahamu, kuna mvutano unaoendelea kati ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa sasa na Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti.

“Sisi tunawaele keza wawakilishi wetu, Prosper Dalali (Chumvi), Rashid Mpamba na Ernest Mgawe kuhakikisha wanawapigia kura, Lissu na Heche,” alisema.

Aliongeza, “tukikosa majiina yao baada ya uchaguzi, watambue kuwa watakutana na hasira za wanachama wa Kibamba”.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Kibamba, Nuru Mcharo alisisitiza kuwa, Lissu na Heche wanahitajika kurejesha misingi ya chama iliyowavutia wanachama kujiunga nacho.

“Hii haimaanishi tunam chukia, Freeman Mbowe au kuona hafai. Mbowe amean dika historia kubwa kama mwanamageuzi mashuhuri, lakini tunaamini ni wakati wa mawazo mapya ili kue ndeleza mageuzi,” alisema Mcharo.

Alisema wanahitaji viongozi wenye dira mpya ili kusukuma mbele ajenda ya chama na kufanikisha mageuzi yanayohitajika kwa maendeleo ya taifa.

Habari Zifananazo

Back to top button