Kampeni Ngoma Juu ya Ngoma yazinduliwa

Kampuni ya Audiomack, imezindua kampeni inayojulikana kama Ngoma Juu Ya Ngoma, inayolenga kukuza ubunifu na kuuza muziki wa kitanzania na itashirikisha wasanii wakubwa wakiwemo Zuchu, Lava Lava, Jux, Barnaba na wengine.

Akizungumza na Daily News Digital, Makamu wa Rais wa Audimack, Jason Johnson, amesema kampeni hiyo itahusisha mabango, redio na matangazo ya kidigitali, matangazo kwenye mabasi, ushiriki wa watu wenye ushawishi.

Amesema katika kukuza uelewa juu ya kampeni hiyo, Audiomack,  ilifanya warsha jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Pia amesema kampeni hiyo itahusisha wamuziki mbalimbali wa kimataifa wa Audiomack, SKYLINE, na maonesho  yanayohusisha tamaduni kutoka Tanzania na kuziweka katika ubora wa juu zaidi.

Amesema Audiomack pia imeshirikiana na kituo cha redio Wasafi FM kilichoshinda tuzo za kuzindua Audiomack Top 10.

“Kipindi hicho kinachorushwa Ijumaa, kinaundwa na chati za Audiomack Top 10 Tanzania zinazoangazia nyimbo kubwa zaidi chini,” amesema.

 

Habari Zifananazo

Back to top button