Kampuni yaaminiwa upimaji madini

KATIKA kukuza sekta ya madini nchini na nje ya nchi kampuni ya kizawa ya Nesch Mintech imeaminiwa na Kampuni ya Madini ya New Future Mining Company ya nchini Saudi Arabia ambapo zinashirikana kupima madini katika maabara lengo kukuza fursa za kiuchumi baina ya nchi zote mbili.
Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Kampuni ya Nesch Mintech Happiness Nesvinga wakati wakisaini makubaliano ya ushirikiano na kampuni hiyo ya New Future Mining Company ya Saudi Arabia ambapo amesema tanzania imeaminiwa na Saudi Arabia hivyo sekta hiyo ya madini inaenda kuleta na kuchachua fursa kwa watu wengi zaidi.
Aidha, Happiness amesema biashara ya vipimo vya madini lengo kuwe na maabara ambapo mchango mkubwa na utekelezaji wa madini umetanuka kwa wigo mpana hivyo ni fursa kwa nchi na jamii nzima.
Naye Mohammed Alomoudi Mkurugenzi wa New Future Mining Company amesema mashirikiano hayo baina ya kampuni hiyo ya kitanzania itadumisha na kutoa ajira kwa vijana wengi hivyo ina tija kwa mataifa yote mawili .
Awali akiongea Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri amesema wanawakinda wawekezaji wazawa katika uwekezaji hivyo ni fahari kwa kampuni ya kizawa kwenda kuwekeza nje ya nchi kwani itafungua fursa baina ya pande zote mbili.