Kansela Scholz ataka sheria za uhamiaji ziheshimiwe

UJERUMANI : KANSELA wa Ujerumani, Olaf Scholz, amesema kuwa haki ya kuomba hifadhi ni jambo la lazima na linapaswa kuheshimiwa.

Ameyasema hayo bungeni wakati ambapo wabunge walikuwa wakijitayarisha kupigia kura muswada unaopendekeza mageuzi katika sera za uhamiaji za Ujerumani.

Muswada huo uliletwa bungeni na Kiongozi wa chama cha upinzani cha CDU, Friedrich Merz, ambaye alisema kwamba atashirikiana na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, AFD, kupitisha mapendekezo yake.

Katika hotuba yake mbele ya Bunge la Ujerumani (Bundestag), ikiwa ni wiki moja baada ya shambulio la kisu katika mji wa Aschaffenburg, kusini mwa Ujerumani, ambalo linadaiwa kufanywa na raia wa Afghanistan.

Kanzela Scholz alisisitiza kuwa haki ya kuomba hifadhi ni sehemu ya misingi ya kisheria ya Ujerumani, na kwamba kanuni zilizopo zinapaswa kulindwa.

Scholz, amesema mikakati inayojumuisha kuwakataa waomba hifadhi katika mipaka ya Ujerumani na kuwanyima uraia wa Ujerumani ni wale ambao wanauraia pacha na wahalifu.

Aliongeza kuwa Ujerumani, kama taifa kubwa barani Ulaya, haitakiwi kuvunja sheria za Umoja wa Ulaya.

Wakatihuohuo,Kansela Scholz alitoa wito wa kuanza kutekeleza hatua za kuwarejesha wahamiaji haramu makwao, huku akisema kuwa wahamiaji watakaokubaliwa kuishi nchini ni wale wenye vibali kwa mujibu wa sheria. SOMA: Polisi ujerumani kuwasaka wahamiaji haramu

Alisisitiza kuwa Ujerumani imeongeza kwa karibu robo moja idadi ya wahamiaji haramu waliorejeshwa nyumbani ukilinganisha na mwaka uliopita.

Amesema pia kuwa Ujerumani inafuatilia kwa karibu hali inayojiri nchini Syria na itaanza mara moja kuwarejesha wahalifu kutoka nchi hiyo wakati hali itakapoimarika.

Hata hivyo, amekiri kwamba ndege moja iliyobeba wahamiaji haramu iliondoka Ujerumani kwenda Afghanistan mwezi Agosti, na nyingine inatarajiwa kuondoka hivi karibuni.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button