UJERUMANI : POLISI nchini Ujerumani inaendelea kufanya msako dhidi ya mtandao wa kihalifu wa wakurdi wenye asili ya Iraq wanaotuhumiwa kusafirisha wahamiaji kwa boti kutoka Ufaransa kwenda Uingereza.
Zaidi ya maafisa 500 waliendesha msako huo kwenye miji kadhaa ya magharibi mwa Ujerumani wakishirikiana na maafisa wengine wa polisi kutoka Ulaya , Europol, na Ufaransa.
Mtandao huo wa wahalifu umekuwa ukisafirisha wahamiaji haramu kutoka Mashariki ya Kati na Afrika Mashariki kuelekea Ufaransa na Uingereza wakitumia mashua mbovu ambazo ni hatarishi kwa maisha ya watu. SOMA: Wahamiaji haramu Ujerumani waongezeka
Miongoni mwa miji iliyokumbwa na msako huo ni Essen, Gelsenkirchen, Grevenbroich na Bochum.