Karia amteua Nyamlani Makamu wa Rais TFF

TANGA; RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amemteua tena Athumani Nyamlani kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa shirikisho hilo.

Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, Rais anateua wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji ambao wanathibitishwa na Mkutano Mkuu wa TFF na miongoni mwa wajumbe ha anatoka Makamu wa Kwanza wa Rais.

Nyamlani ametangazwa leo kushika wadhifa huo kwenye Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika jijini Tanga ikiwa ni awamu ya pili, ambapo mara ya kwanza aliteuliwa mwaka 2021.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button