Karia: Asanteni, chuma kimepita kwenye moto

TANGA; RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amewashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo na kuwataka wasisikitike na yaliyojitokeza kwenye mchakato wa uchaguzi wa shirikisho hilo, badala yake waende wakachape kazi.

Akizungumza leo Agosti 16, 2025, baada ya kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa TFF kushika wadhifa huo kwa miaka minne ijayo, amesema kilichotokea ilikuwa chuma kinapitishwa kwenye moto ili kiwe imara.

Amewataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kuendelea kutekeleza majukumu yao ipasavyo, kwani kama uongozi wa juu ukifanya vizuri halafu ngazi ya chini mambo hayaendi itakuwa sawa na bure.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button