Katibu Mkuu ujenzi aagiza Tanroads kupunguza msongamano Dar

DAR ES SALAAM: Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour, ameuelekeza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kufungua kwa muda barabara zote za makutano katika maeneo yanayotekelezwa miradi ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) ili kupunguza msongamano wakati ujenzi ukiendelea.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo jijini Dar es Salaam, Balozi Amour alisema hatua hiyo imelenga kupunguza msongamano wa magari kuelekea kipindi cha Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, ambacho kwa kawaida huongeza idadi ya watu na magari jijini humo.
“Tumeona njia ya haraka ya kupunguza msongamano katika kipindi hiki ni kufungua barabara za makutano wakati tukisubiri ujenzi wa kudumu wa barabara hizo unaoendelea, ikiwemo ule wa BRT”.

Aidha, ameelekeza wakandarasi wote kuhakikisha kuwa barabara za michepuko zinapitika na ziko katika hali nzuri. Amesema kuwa mkandarasi anayejenga kipande cha barabara ya Mwenge–Tegeta ameahidi kuweka lami ya muda katika barabara ya mchepuko ili kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji.

Balozi Amour ameongeza kuwa ili kupunguza malalamiko yanayotokana na msongamano unaosababishwa na utekelezaji wa mradi wa BRT, TANROADS itatoa taarifa za mara kwa mara ili kuwasaidia watumiaji wa barabara kujua njia mbadala yakutumia wakati wa kwenda na kurudi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Ametoa wito kwa wananchi kufuata sheria za usalama barabarani, ikiwemo kuzingatia vibao vya muda vitakavyowekwa katika maeneo husika.

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Alinanuswe Kyamba, amesema tayari wameanza kuyafanyia kazi maelekezo ya Katibu Mkuu na wamewaelekeza baadhi ya wakandarasi kuanza kufungua barabara hizo.




Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
.
Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com