Katimba-Uchaguzi upite,umoja ubaki

KIGOMA: NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Katimba, amewataka Watanzania kutokubali kupoteza amani yao au kufarakana kutokana na tofauti za kisiasa zinazojitokeza wakati wa uchaguzi.

Amesema kuwa chaguzi ni za muda na hupita, lakini mahusiano ya kidugu na kitaifa ni ya kudumu na ndiyo msingi wa mshikamano wa taifa. Akizungumza akiwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) yaliyoandaliwa na Msikiti wa Muumin, Ujiji mkoani Kigoma, Katimba amewahimiza Watanzania kushiriki michakato ya uchaguzi kwa amani bila ugomvi.

Naibu Waziri huyo alisisitiza kuwa serikali imeweka sheria na taratibu za uchaguzi ambazo kila mmoja kuanzia wagombea, viongozi wa vyama hadi wananchi wa kawaida anatakiwa kuzingatia. Amesema uchaguzi wa kistaarabu unahitaji kila mtu kusimama kwenye nafasi yake, kufanya maamuzi kwa busara na kuepuka jazba. SOMA: Amani iendelee kutawala kampeni Uchaguzi Mkuu

Naye Kadhi wa Mkoa Kigoma, AbdulMuhsin Kitumba, alisema Maulid ni siku muhimu kwa Waislamu duniani kote, kwani ni fursa ya kukumbuka na kuenzi maisha mema na mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW), ambayo waumini wanapaswa kuyaishi kila siku.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button