Kavejuru asaidia ujenzi wa ofisi ya CCM

KIGOMA: MBUNGE wa jimbo la Buhigwe wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Felix Kavejuru ametoa msaada wa bandari 12 za bati kwa ajili ya kusaidia kumalizia ujenzi ya ofisi ya CCM ya wilaya hiyo.

Kavejuru amekabidhi bati hizo zenye thamani ya shilingi milioni 5.9 kwa Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi ya ofisi hiyo,Silvestre Kigwinya na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa CCM wilaya Buhigwe.

Amesema msaada huo umelenga kuunga mkono juhudi za viongozi wa wilaya hiyo kuwa na ofisi yao yenye hadhi ya wilaya kuondoka katika jengo la kuazima.

Advertisement

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya kamati ya ujenzi, Mwenyekiti wa kamati hiyo Silvestre Kigwinya ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Buhigwe amesema msaada huo utawezesha mradi wa ujenzi wa ofisi hiyo kupiga hatua kubwa.

SOMA: Kiruswa achangia Sh milioni 15 Ujenzi ofisi ya CCM Longido

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya Buhigwe, Erneo Dyegula amemshukuru Mbunge Kavejuru kwa msaada huo wa mabati kuunga mkono juhudi za ujenzi wa jengo hilo la ofisi ya CCM wilaya Buhigwe kwani litawafanya kuwa na ofisi yao kuondoka katika ofisi ya kuazima ya CCM kata ya Buhigwe ambayo wanatumia sasa.