Wafanyakazi wa anga watishia mgomo

KENYA : CHAMA cha Wafanyakazi wa Usafiri wa Anga nchini Kenya (KAWU) kimetoa notisi ya siku saba cha kutishia mgomo iwapo Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (KAA) haitajiuzulu. Wamesema bodi hiyo imeshindwa kushughulikia maslahi ya wafanyakazi na mkataba wa kukodisha uwanja wa ndege.

Mgomo huo unaweza kuathiri shughuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, ambao ni kitovu muhimu cha safari za anga barani Afrika. Katibu Mkuu wa KAWU, Moses Ndiema, amesema mgomo unaweza kuanza mara baada ya notisi kumalizika. SOMA: Mgomo wiki saba Boeing wamalizika

Hii si mara ya kwanza kwa wafanyakazi wa viwanja vya ndege kugoma. Mwaka jana waligoma kupinga mpango wa kukodisha uwanja kwa kampuni ya Adani Group, mpango uliofutwa baadaye.

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button