MAREKANI : WAFANYAKAZI wa Boeing wamepiga kura kwa asilimia 50% ya kukubali ofa ya malipo mpya ya kampuni hiyo na kumaliza mgomo wa wiki saba.
Kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba mpya imeongeza nyongeza za mishahara kwa asilimia 38% katika kipindi cha miaka minne.
Mgomo huo ulihusisha wafanyakazi 30,000 wa Boeing na ulianza Septemba mwaka huu ambapo ulisababisha hasara katika upande wa makusanyo ya mapato.
Hatahivyo, Chama cha wafanyakazi wa anga kimesema asilimia 59% ya wafanyakazi waliogoma walipiga kura kuunga mkono mpango huo mpya uliojumuisha malipo ya marupurupu ya dola za kimarekani $12,000 sawa na euro (£9,300) kwa kila mmoja na kukubali kufanya maboresho ya malipo kwa wafanyakazi wastaafu.