Boeing 8787-8 Dreamliner kufika leo
ZANZIBAR : Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawajulisha wananchi kwamba ndege mpya ya Boieng 8787-8 Dreamliner inatua leo ikitokea nchini Marekani.
Ndege hii ilishindwa kuwasili jana kutokana na changamoto za hali ya hewa.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Ikulu Zanzibar imesema kuwa ndege ya Boeing 8787-8 itawasilia majira ya saa kumi jioni katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Abeid Amani Karume na itapokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi .
Ofisi ya Ikulu Zanzibar imewaomba wananchi wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi kuipokea ndege Boeing 8787-8 Dreamliner .
SOMA: Dreamliner yashindwa kufika Zanzibar
#UPDATES