Dreamliner yashindwa kufika Zanzibar
ZANZIBAR : Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar SMZ inasikitika kuwajulisha wananchi kwamba ndege aina ya Boeing 8787-8 Dreamliner, ambayo iliyotarajiwa kufika na kutua leo katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume imeshindwa kufika kutokana na changamoto za hali ya hewa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Ikulu Zanzibar leo imesema mapokezi na uzinduzi wa ndege hiyo ya Boeing 8787-8 Dreamliner ilipangwa kufanywa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Taarifa hiyo imesema kuwa ratiba nyingine ya mapokezi ya ndege hiyo yataweza kutolewa tena baadaye hadi utakapokamilika na kuwaomba radhi wananchi wa Zanzibar na wengine kwa usumbufu woowte uliojitokeza.
SOMA : Serikali yapewa ushari kuepuka hasara ATCL