Kazi na utu ndio mtihani wa mawaziri

KUAPISHWA kwa mawaziri na naibu mawaziri jana ni hatua muhimu katika safari ya kuijenga Tanzania yenye ufanisi, umoja na maendeleo.
Akizungumza kwenye hafla ya kuwaapisha jana Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Rais Samia Suluhu Hassan aliwapongeza lakini akaweka bayana kwamba mbele yao kuna kazi kubwa, nzito na inayohitaji uwajibikaji kwa ajili ya wananchi.
‘Kazi na Utu, Tunasonga Mbele’ ni dira inayopasa kuwaongoza katika utekelezaji wa majukumu yao kwa maana ya kufanya kazi kwa weledi, kwa kujituma na kwa kuzingatia thamani ya binadamu.
Kwa maneno mengine, uwaziri ni dhamana ambayo mawaziri wanapaswa kutotambia wadhifa huo wa juu serikalini, bali kushuka na kuonesha matokeo chanya kwa wananchi.
SOMA: Serikali ya kasi
Rais Samia amefanya sehemu yake kwa kuwaamini na kuwakabidhi wizara, akiamini watamsaidia na sasa ni zamu yao kuhakikisha wanaandika alama chanya kwenye maisha ya Watanzania.
Ni jukumu lao kuthibitisha bila shaka kwamba hawakuteuliwa isivyo bahati, bali ni kutokana na uwezo wao wa kuongoza na kuleta mabadiliko.
Kama alivyowausia Rais Samia na sisi tunasisitiza kwamba wananchi hawahitaji maneno, bali wanataka suluhu ya changamoto zao na matokeo yanayoonekana.
Kila aliyeapa ahakikishe anajiandaa kwenda na kasi ya Rais Samia kwa kuacha urasimu usio wa lazima na kufanya kazi kwa kasi, maarifa na moyo wa kujali maslahi ya wengi.
Ni wazi, katika kipindi ambacho dunia inabadilika kwa kasi kutokana na sayansi na teknolojia, changamoto za wananchi zinahitaji mawaziri wanaoweza kusimama imara, kusikiliza, kupanga, kutekeleza na kufuatilia.
Aidha, mawaziri wazingatie usia wa Rais Samia wa kuhakikisha hawaubebi uwaziri kama fahari ya kutamba mitaani, bali wautumie kutenda haki kwa kila Mtanzania kwa utu, bila upendeleo, ubaguzi na bila kujiona wao ni wa daraja tofauti. Utu ndiyo silaha ya kuleta heshima ya kweli ya utumishi wa umma.
Tunawakumbusha mawaziri kwamba sasa ni wakati wa kufanya kazi kwa bidii na kwa utu, kwani wananchi wanawaangalia na rais aliyewaamini anawasubiri.
Matokeo yao yataonekana katika maisha ya watu na si kwenye maneno.
‘Kazi na Utu, Tunasonga Mbele’ iwe dira kwa kila mmoja katika kutekeleza majukumu. Pia, falsafa hii iwe ni mtihani wa mawaziri hawa wapya ambao matokeo yake yanapaswa kuonekana katika ustawi wa Watanzania wote bila kujali tofauti zao.
Tunaungana na Rais Samia aliyewapongeza mawaziri, huku akiwahadharisha kwamba wana kazi kubwa mbele yao.




Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us →→→→→→→ https://Www.Work27.Online
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting website
More Details For Us→→ http://www.job40.media