KENYA : BENKI ya Dunia imepunguza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa Kenya kwa mwaka huu hadi asilimia 4.7 kutoka asilimia 5.0 kutokana na athari za mafuriko, maandamano ya kuipinga serikali na juhudi za kuimarisha fedha.
Taifa hilo la Afrika Mashariki limefanikiwa kuimarisha kiwango chake cha ubadilishaji wa fedha za kigeni, kuongeza akiba ya fedha taslimu katika benki kuu na kupunguza mfumuko wa bei mwaka huu, lakini bado inakabiliwa na hatari kubwa ya kukumbwa na madeni.
“Ingawa makadirio ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2024 umekuwa chini kuliko kiwango cha mwaka jana cha asilimia 5.6%, bado ukuaji huo ni wa juu kuliko wastani wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao ni asilimia 3.0%,”ripoti ya benki ya dunia ilisema.
Ukuaji wa uchumi wa Kenya unaweza kufikia asilimia 5.1 katika kipindi cha kati ikiwa serikali itafanikiwa kukabiliana na changamoto za kifedha. SOMA: IMF yaiomba Kenya kuchunguza ufisadi