KENYA: Wanawake 200 wapoteza maisha 2024

KENYA : IMEELEZWA kuwa karibu wanawake 200 waliuawa nchini Kenya mwaka jana, katika matukio ya ukatili wa kijinsia.

Idadi hii ambayo ni karibu mara mbili ya ile ya mwaka uliopita imetolewa na makundi yanayofuatilia vitendo hivyo. SOMA: Kenya yapinga mauaji wanawake

Ripoti ya kila mwaka ya kundi linalopambana na vitendo vya kuwanyamazisha wanawake kwa ushirikiano na kampuni ya data ya Odipo Dev pamoja na chombo cha habari cha Africa Uncensored, iligundua kuwa wanawake 170 waliuawa mwaka jana, kutoka 95 mwaka uliopita.

Mtafiti mkuu wa kundi hilo Patricia Andago amesema mwaka 2024 ulikuwa mwaka mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa wanawake wa Kenya, na kwa bahati mbaya hakuna dalili zozote zinazoashiria kuwa vitendo hivyo vitapungua.

Suala la unyanyasaji wa kijinsia limeenea katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, ambapo mwaka jana polisi walifyatua mabomu ya machozi  wanaharakati walipojaribu kuandamana katika mji mkuu wa Nairobi wakitaka kukomeshwa kwa mauaji ya wanawake.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button