ISRAEL : WAZIRI Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewasilisha ushahidi mahakamani leo wa tuhuma za rushwa.
Waendesha mashtaka nchini humo wamemshutumu kiongozi huyo kwa kutoa makubaliano ya kisheria kwa wamiliki wa vyombo vya habari ili kupata habari chanya na kukubali zawadi na faida za gharama kubwa kwa lengo la kuendeleza maslahi binafsi.
Netanyahu atakuwa ni kiongozi wa kwanza nchini humo kuwasilisha ushahidi kama mshtakiwa katika kesi ya jinai. SOMA: Israel kukata rufaa dhidi ICC
Pia amejaribu kuchelewesha mchakato huo kutokana na vita vya Gaza na wasiwasi wa kiusalama lakini wiki iliyopita majaji waliamuru kesi hiyo ya madai ya rushwa iendelee.
Hivi karibuni ,majaji katika Mahakama ya kimataifa ya uhalifu nao walitoa waranti maalum ya kukamatwa Benjamin Netanyahu kwa makosa ya uhalifu wa kivita.