Kesi ya wanafamilia kusikilizwa upya Moshi

JAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi,Lilian Mongella ameliagiza Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi la mji wa Moshi kusikiliza upya kesi ya wanafamilia maarufu katika ya Chief Mareale ya kugombea ardhi ya ekari mbili.

Ardhi hiyo ipo kijiji cha Lyamrakana Marangu na kusema kuwa baraza lilikosea kisheria wakati walipotembea eneo la tukio la mgogoro wa ardhi kwani halikuonyesha mipaka ya eneo husika.

Watoto Chief Mareale waliofikishana mahakamani ni Frank Mareale dhidi ya Ackley Mareale kwani Frank anadai eneo hilo ni mali yake aliishi miaka zaidi ya 43 na Ackley anadai mama yake Veronica Mareale aliishi eneo hilo na kuzikwa mwaka jana kwa zaidi ya miaka 80.

Akisoma hukumu hiyo leo Jaji Mongella alisema baada ya kupitia ushahidi na maamuzi ya Baraza la Nyumba na Makazi la Mji wa Moshi chini ya uenyekiti wa Reginal Mtei yaliyotolewa Mei 5 mwaka huu maamuzi hayo yalikuwa na kasoro za kisheria hivyo aliagiza baraza hilo kusikiliza kesi upya.

Jaji Mongella alisema moja ya mapungufu katika maamuzi ya baraza ni pamoja na kushindwa kuonesha au kurekodi mipaka ya ardhi ya ekari mbili inayogombaniwa na wanafamilia hao hivyo ametengua maamuzi hayo na kuamuri kesi hiyo isikilizwe upya chini ya mwenyekiti na wajumbe wengine wapya.

Alisema katika mapitio ya maelezo ya mashahidi wa kesi hiyo katika Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi hakuona kama Baraza hilo limeonyesha mipaka ya eneo lenye mgogoro na kusema kuwa kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

“Nimeamua kesi hii ya wanafamilia wa Chief Mareale isikilizwe upya kwa sababu Baraza la Ardhi lilikosea kisheria kwa kushindwa kuonyesha mipaka ya ekari mbili inayogombaniwa.” alisema Jaji Mongella

Katika kesi iliyofunguliwa na Frank Mareal katika Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi katika mji wa Moshi, alikuwa na madai matatu moja wapo ni kulitaka Baraza hilo litamke kuwa eneo la ekari mbili yeye ni mmiliki halali, pili baraza litoe amri ya kufukuliwa mwili wa marehemu mama yake mdogo Veronica Mareale na pia alipwe gharama za kesi.

Mei 5 mwaka huu chini ya uenyekiti wa Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi Reginald Mtei lilitupilia mbali madai ya Frank Mareale na kusema kuwa Ackley Mareale ni mmiliki halali wa eneo hilo na sio vinginevyo.

Akizungumza nje ya mahakama, wakili wa Ackley Mareale,Julius Semali alisema kuwa hana pingamizi na uamuzi wa mahakama kwani ana uhakika kuwa mteja wake ni mmiliki halali  wa eneo hilo kwa kuwa mama yake alipata kihalali eneo hilo na alizikwa ene hilo na kurudishwa tena katika baraza hana shaka na uamuzi wa awali na kusema kuwa usikilizwaji mwingine utathibitisha kuwa haki ya mtu huwa haipotea ila inacheleweshwa.

Naye Wakili wa frank Mareale,Modest Njau aliishukuru Mahakama Kuu kwa uamuzi wake wa kuiagiza Baraza la Ardhi Nyumba na MakaziMoshi kusikiliza upya kesi hiyo  na aliamuru Mwenyekiti wa Baraza na wajumbe wake wabadilishwe.

Njau alidai Mahakama Kuu iliona jinsi haki ilivyokuwa ikitaka kuchezewa katika usikilizwaji wa awali na yeye na mteja wake wameridhika na maamuzi hayo.

Habari Zifananazo

9 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button