Kibaha watakiwa kulinda vyanzo vya maji

PWANI; Kibaha. Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson Saimon amesema ili kuondokana na kikwazo cha ukosefu wa maji kwenye baadhi ya maeneo, jamii inatakiwa kujenga tabia ya kulinda vyanzo vya maji badala ya kuacha kazi hiyo kufanywa na serikali pekee.

Saimon amesema kila mmoja anatakiwa kwenye eneo lake kuwa mlinzi wa vyanzo vya maji sambamba na miundombinu inayojengwa, ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Amesema suala la maji likiachwa kwa serikali peke yake ni kutengeneza  jamii ambayo haina uwajibikaji ili hali kila mmoja anatakiwa katika eneo lake kulipa bili kwa wakati, kulinda vyanzo vya maji na kutoa taarifa inapotokea hitilafu.

Mkuu huyo wa Wilaya aliyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha nusu mwaka cha wadau wa sekta ya maji kilichoandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)  katika Halmashauri ya Kibaha Vijijini.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kibaha, Mhandisi Debora Kanyika amesema kwa sasa huduma ya maji imeimarika na tayari vijiji 25 kati ya 26 vimefikiwa.

Mhandisi Debora amesema miradi yote iliyokamilika inawanufaisha watu 100,220 na kuinua hali ya upatikanaji wa maji kwa miaka 11 na kufanya ongezeko la wanaopata huduma ya maji kufikia asilimia 78 kutoka 67 ya mwaka 2019.

Kwa mujibu wa Meneja huyo ifikapo Juni 2024 asilimia kubwa ya wakazi wa Kibaha Vijijini watakuwa na huduma ya maji safi na salama kupitia uteekelezaji wa  miradi ya bajeti ya mwaka huu.

Mmoja wa washiriki wa kikao hicho, ambaye ni Diwani Viti Maalumu Josephine Gunda ameomba mamlaka hiyo kuendelea kutenga bajeti kwa ajili ya miradi mikubwa iliyokamilika ili marekebisho yaendelee kufanyika maeneo yenye vikwazo.

Gunda pia ameomba RUWASA kuzingatia idadi ya wanufaika kwenye maeneo wanayounganisha maji ili yakidhi mahitaji sambamba na kuyafikisha maeneo ya Vitongoji.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Work AT Home
Work AT Home
1 month ago

I make $100h while I’m daring to the furthest corners of the planet. Last week I worked by my PC in Rome, Monti Carlo finally Paris… This week I’m back in the USA. All I do are basic tasks from this one cool site. see it, 
Copy Here→→→→→ http://Www.Smartcash1.com

Last edited 1 month ago by Work AT Home
KimmieJules
KimmieJules
1 month ago

★They pay me $285 per hour to work on a laptop. ( g00q) I had no clue it was possible, but a close friend made $26,000 in four weeks working on this simple offer, and she convinced me to try it. For further information, please see.
Click and Copy Here══════►►► http://Www.SmartCareer1.com

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x