Kihongosi atembelea miradi Karatu

ARUSHA: Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi amekuwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali pamoja na kuzungumza na watumishi wa umma na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi kupitia mikutano ya hadhara wilayani Karatu.

Katika ziara hiyo, RC Kenani ametembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karatu ambapo Serikali Kuu imetoa Sh milioni 800 kwa mwaka wa fedha 2025/26 kuendeleza miundombinu na ununuzi wa vifaa tiba katika hospitali hiyo.

Awali, akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo wakati wa mapokezi yake kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, RC Kihongosi ameipongeza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo kwa kuendelea kuimarisha usalama kwa wananchi pamoja na watalii wanaotumia Mji wa Karatu kama lango la kuingia kwenye Hifadhi za Taifa za Serengeti pamoja na Ngorongoro.

Kwa upande wao wananchi wanufaika wa hospitali hiyo, akiwemo Joseph Akonay na Elizabeth Qoro wameishukuru serikali kwa ujenzi wa hospitali hiyo huku wakieleza kuwa awali walikuwa wakifuata huduma za afya mbali na kutumia gharama kubwa za usafiri huku vifo vya mama na mtoto vikiwa vingi kutokana na wengi kujifungulia njiani kutokana na umbali mrefu waliokuwa wakisafiri awali kufuata huduma za afya.

Kihongosi apiga marufuku ‘faini ya funguo’ Arusha

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button