Kijana auawa kwa bomu kilabuni

MKULIMA mkazi wa kijiji cha Basanza wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma amefariki dunia baada ya kulipuliwa na bomu la kurusha kwa mkono lililorushwa ndani ya kilabu cha pombe wakati akinywa na wenzake.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma, Filemon Makungu alisema mjini Kigoma kuwa aliyeuawa kwenye tukio hilo ni Amos Petro (45) na watu wengine wawili walijeruhiwa.

buy flagyl online qualitydentistry.com/library/dlinks/html/flagyl.html no prescription pharmacy

Kamanda Makungu alisema Petro alifariki dunia kwenye Hospitali ya Wilaya Uvinza wakati akipata matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya mguu wa kushoto na kuvuja damu nyingi.

buy addyi online qualitydentistry.com/library/dlinks/html/addyi.html no prescription pharmacy

Aidha kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Juma Omari (51) na Sara Misigaro wakazi wa kijiji cha Basanza ambao wako hospitali ya wilaya Kasulu wakipatiwa matibabu.

buy inderal online qualitydentistry.com/library/dlinks/html/inderal.html no prescription pharmacy

Kamanda Makungu alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo mtu mmoja alirusha bomu hilo kwenye kilabu cha pombe za kienyeji wakati Petro na wenzake wakinywa pombe

Alisema uchunguzi wa awali umeonesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia na hivyo upelelezi unaendelea ili kuwakamata na kuwachukulia hatua  wanaohusika.

Habari Zifananazo

Back to top button