Kikwete ampa 5 Rais Samia

RAIS Mstaafu wa awamu ya nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete amepongeza Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia katika ngazi zote ambayo yameongeza idadi ya wanafunzi wasichana hata kwenye masomo ya sayansi ambayo awali yalionekana kuwa ni ya wavulana pekee.

Ametoa pongezi hizo leo katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu Mkwawa cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akiwatunuku wahitimu 1,578 wa Shahada za Udhamili na Shahada za Awali, Dk Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema ongezeko la wanafunzi wasichana katika elimu na hasa ya juu ni jambo la kupongeza na kuendelezwa zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki Cha Elimu Mkwawa, Prof William Anangisye ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amewataka wahitimu hao kuwa wabinifu na kuchangamkia mikopo inayotolewa na Halmashauri mbalimbali nchini badala ya kusubiri ajira za Serikali.

Habari Zifananazo

Back to top button